Wednesday, 19 June 2013

THAMANI YA UHAI NA HARAKATI

UHAI WA MWANADAMU NI ZAWADI NA TUNU BORA SANA TULIYOPEWA MARA MOJA NA DAIMA.JUKUMU LA KULINDA UHAI WAKO NA WANGU NI LANGU NA LAKO KWANZA KABLA YA KUNYOOSHEANA VIDOLE.HATA HIVYO KAMA KUNA AINA YOYOTE YA UZEMBE KWAKO WEWE KIJANA YA KUJIKINAI AU KUWAKINAI WENGINE BASI ULINZI WA UHAI WAKO LAZIMA UTAGHARIMU KIZAZI CHA SASA NA KIJACHO.HATUPASWI KURUHUSU MIHEMKO YETU KUTAWALA BONGO ZETU HADI KUKOSA SUBIRA NA FADHILA YA UVUMILIVU  HADI KUUVAA UNYAMA NA KUJIVIKA MAUTI.INATIA HUZUNI KWA VIJANA KUPOTEZA UHAI WAO KATIKA JINA LA HARAKATI NA NEMBO YA VYAMA VYA SIASA.TUKUMBUKE UHAI TUNAO MARA MOJA NA DAIMA BALI HARAKATI HII IKIISHA HUIBUKA NYINGINE.TUSOME ALAMA ZA NYAKATI HIZI ZA MASHETANI WANAOTAWALA DUNIA KUPITIA DAMU YA WANYONGE WENGI.MASIKINI MLIOPOTEZA UHAI WENU MKIDHANI MTAKUMBUKWA BADAALA YAKE MTASAHAULIWA MILELE KWANI NGAZI IKISHA MKWEZA MKWEZI HAISHUKURIWI BALI MKWEZI HUPONGEZWA TU!!TUSIKUBALI KUWA NGAZI UCHWARA.

BINAFSI NAPENDA SIASA LAKINI SIO FUJO ZA CHADEMA WALA KUKOSA UVUMILIVU KWA CCM.MJIREKEBISHE WOTE.

0 comments:

Post a Comment